top of page

Miongozo

Kwa Manufaa ya Wote

  1. Heshima na Pole: Watendee washkaji wote kwa heshima na wema. Epuka mashambulizi ya kibinafsi, matusi, au lugha ya dharau.

  2. Mawasiliano ya Kujenga:Shiriki katika mijadala yenye kujenga na toa maoni yenye manufaa. Kutokubaliana kunakubalika, lakini kila wakati toa maoni kwa njia ya heshima.

  3. Hakuna Ubaguzi:Usiwabague au kuwanyanyasa wengine kwa misingi ya rangi, jinsia, dini, utaifa, mwelekeo wa kingono, au tabia nyingine yoyote ya kibinafsi.

  4. Faragha na Usiri:Heshimu faragha na usiri wa wengine. Usitoe maelezo ya binafsi ya wanachama wa Vijiwe bila ridhaa yao.

  5. Hakuna Barua taka au Utangazaji: Epuka kutuma barua taka, kujitangaza kupita kiasi, au matangazo yasiohusu. Maudhui yoyote ya utangazaji yanapaswa kuwa muhimu nakupitishwa na wasimamizi wa jukwaa.

  6. Kaa kwenye Mada:Weka mijadala inayoendana na kategoria za jukwaa na mada. Epuka kutoka nje ya mada kupita kiasi.

  7. Hakuna Wizi au Ukiukaji wa Hakimiliki: Usichapishe maudhui ambayo yanakiuka sheria za hakimiliki au kuiga kazi za wengine. Toa credit kila wakati unapotuma maudhui ya mtg mwingine.

  8. Hakuna Maudhui Haramu: Kuchapisha au kushiriki maudhui haramu au hatari, ikijumuisha, lakini sio tu, nyenzo chafu, programu potofu, au viungo hasidi, ni marufuku kabisa.

  9. Kuwa mwangalifu na Lugha: Tumia lugha ifaayo na uepuke kutumia lugha chafu kupita kiasi au lugha ya kuudhi ambayo inaweza kuharibu mazingira chanya ya jukwaa.

  10. Kuripoti Masuala: Ukikutana na ukiukaji wowote wa sheria za mijadala, ripoti kwa wasimamizi mara moja.

  11. Kuzingatia Sera za Mijadala: Jifahamishe na ufuate sera zote za mijadala, sheria na masharti na miongozo.

bottom of page